Folge uns
iBookstore
Android app on Google Play
Gefällt mir
Ein Programm der Universität Leiden
Mwanga Toka Gizani
16. January 2013

Sio mara zote vitu huwa kama vinavyoonekana, haswa huko angani. Sehemu za wazi zilizopo angani mara nyingi huficha siri nzuri za kusisimua. Picha hii mpya inaonyesha gimba la wingu la vumbi linalowaka karibu kabisa na nyota ing’aayo. Ukingalia kwa  macho sehemu hizi huonekana kuwa na giza na kama hazina kitu chochote, lakini baadhi yake ni sehemu ambapo magimba ya Nebula na nyota changa hupatikana!

Nyota zinatengenezwa kutokana na gesi, hivyo haishangazi kama zinazaliwa ndani ya gimba nene la wingu la gesi. Lakini mawingu yanayosababisha kuzaliwa kwa nyota hutukinga kuona jinsi zinavyowaka ndani yake. Lakini imekuwa ni bahati kwetu kwani kwa jinsi nyota inavyozidi kuungua na kung’aa huunguza pia gesi zinazoizunguka na kufanya vyote viweze kuonekana. 

Kundi la nyota zenye kung’aa lililopo katikati kabisa ya picha ni mfano mzuri wa jambo hili. Miale yake ya blu inaweza kuonekana kwa urahisi sana na kutopotea katika michirizi miyeusi ya gesi inayoizunguka. Nyota mbili zinazong’aa sana katika picha zinaweza kuonekana kwenye usiku wenye giza kubwa kwa kutumia darubini. Hizi ni nyota mbili changa, zenye umri chini ya miaka milioni moja — katika miaka ya nyota huu umri ni mdogo sana na kama ni mtoto basi hata kutambaa bado hajaanza.

Dokezo

Sehemu nyota inapozaliwa kama hii inaweza kuwa kubwa mno! Kwa mfano, Nebula ya Tarantula ambayo unaweza kuiona hapa ina mamia ya nyota kubwa ambazo zinatengenezwa. Kama ukiweza kuindanganya fizikia na kusafiri katika mwendo wa mwanga basi itakuchukua miaka 650 kuikatiza! 

Share:

Mehr Neuigkeiten
14 September 2020
10 September 2020
3 September 2020

Bilder

Licht aus der Dunkelheit
Licht aus der Dunkelheit

Printer-friendly

PDF File
1,1 MB