Folge uns
iBookstore
Android app on Google Play
Gefällt mir
Ein Programm der Universität Leiden
Kuainisha Mipaka ya Galaxi
16. May 2012

Miale ya mwanga kutoka katika nyota zaidi ya billion katika galaxi imeungana katika picha hii mpya yenye mngao pevu. Ni vigumu kuona umbo la galaxi hii kwa sababu mwanga wake hufifia kadri unavyosogea mbali kutoka kwenye kiini chake, na kufanya mipaka yake iseleweke katika kingo zake.

Ili kutambua umbo la galaxi hii, kwanza kabisa bofya katika picha ili uione katika ukubwa halisi. Kisha tengeneza fikra kama unachora mpaka nje ya mngao wa mwanga kwa kutumia kalamu nyeusi. Unaweza kugundua kuwa ina umbo la yai au mpira wa rugby. Wanaangana wanaziita galaxi zenye umbo kama hilo eliptiko (elliptical). Pia kuna galaxi ambazo zinaonekana kama shimo maji (whirlpools) angani ambazo zinaitwa spiral galaxi (galaxi mzunguko), lakini kuna galaxi nyingine nyingi ambazo zina maumbo tofauti (Galaxi yetu ya Milkway “Njia Maziwa” ina umbo kama la mzunguko)

Eliptiko ni galaxi ambazo ndizo kubwa zaidi katika ulimwengu, nyota zake zinakizunguka kiini chake katika pande tofauti tofauti. Hii inafanya eliptiko galaxi ziwe tofauti na spiral galaxi ambapo nyota zote hukizunguka kiini na hukizunguka katika ukanda mmoja usioonekana.  Kwa ujumla eliptiko galaxi ni kama yai au mpira wa ruby, wakati spiral galaxi ni nyembamba kama sahani nyembamba.

Ila tofauti na spiral galaxi, eliptiko hazina vumbi, ingawa eliptiko galaxi ya kwenye picha ina kiasi kidogo cha vumbi, ambacho kinaweza kuonekana kama ukanda wa mawimbi (wavy) kukatiza kati kati. Wanaanga wanadhania kuwa huenda ukanda huo ukawa ni mabaki ya spiral galaxi iliyosambaratishwa na nguvu kubwa ya uvutano (gravity) kutoka kwa eliptiko galaxi!

Dokezo

Ili kukusanya mwanga wa kutosha kutoka kwenye galaxi, picha hii ilichukua masaa 50 kuipiga! Huo ni mda mrefu kwa kutabasamu kwenye picha!

Share:

Mehr Neuigkeiten
14 September 2020
10 September 2020
3 September 2020

Bilder

Galaktische Grenzen markieren
Galaktische Grenzen markieren

Printer-friendly

PDF File
1,0 MB